إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٞۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلٗا ٦٥
Inna 'ibādī laysa laka 'alayhim sultānun wakafā birabbika wakīlā
Hakika wewe huna mamlaka juu ya waja wangu. Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni wa kutegemewa. 65
Maelezo ya chini
65 Ama waja wangu walio nisafia niya Mimi wewe huna uwezo wa kuwapotoa, kwa kuwa wao wanamtegemea Mola wao Mlezi. Na Yeye anatosha kabisa kuwa ni wa kuwanusuru wakimtaka msaada wa kusalimika nawe.