Surat Al-Isra, aya 15

17:15

مَّنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبۡعَثَ رَسُولٗا ١٥

Mmanihtadā fa innamā yahtadī linafsihī waman dalla fa innamā yadillu 'alayhā walā taziru wāziratun wizra ukhrā wamā kunnā mu'addhibīna hattā nab'atha rasūlā

Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. 15

Maelezo ya chini

15 Mwenye kufuata njia ya Haki basi anajifaa mwenyewe, na mwenye kuiacha basi anajipoteza mwenyewe. Wala hapana mwenye kubeba dhambi zake akambebea dhambi za mwenginewe. Wala haitufalii kumuadhibu yeyote kwa kutenda kitu kabla hatujampelekea Mtume kutoka kwetu amwonyeshe njia ya Haki na kumkataza maovu.