Surat Al-Isra, aya 16

17:16

وَإِذَآ أَرَدۡنَآ أَن نُّهۡلِكَ قَرۡيَةً أَمَرۡنَا مُتۡرَفِيهَا فَفَسَقُواْ فِيهَا فَحَقَّ عَلَيۡهَا ٱلۡقَوۡلُ فَدَمَّرۡنَٰهَا تَدۡمِيرٗا ١٦

Wa idhā aradnā an nuhlika qaryatan amarnā mutrafīhā fafasaqū fīhā fahaqqa 'alayhal-qawlu fadammarnāhā tadmīrā

Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa. 16

Maelezo ya chini

16 Na pindi tukikadiria tangu azali katika Lauhun-mahfuudh kuwateketeza watu wa mji fulani kwa mujibu wa hikima yetu, basi Sisi huwasalitisha wale walio jidekeza kwa taanusi katika huo mji, wakafanya fisadi zao, wakaacha njia ya Haki, na wakawafuata wenginewe bila ya kutambua, na kwa hivyo huo mji wote tena hapo hustahiki kuangamizwa. Nasi huuangamiza vikubwa mno!