وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ ءَايَتَيۡنِۖ فَمَحَوۡنَآ ءَايَةَ ٱلَّيۡلِ وَجَعَلۡنَآ ءَايَةَ ٱلنَّهَارِ مُبۡصِرَةٗ لِّتَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡ وَلِتَعۡلَمُواْ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلۡحِسَابَۚ وَكُلَّ شَيۡءٖ فَصَّلۡنَٰهُ تَفۡصِيلٗا ١٢
Waja'alnal-layla wan-nahāra āyatayni famahawnā āyatal-layli waja'alnā āyatan-nahāri mubsiratal litabtaghū fadlam mir rabbikum walita'lamū 'adadas-sinīna wal-hisāba wakulla shay'in fassalnāhu tafsīlā
Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi. 12
Maelezo ya chini
12 Na Sisi tumejaalia usiku na mchana, kwa namna yao na kupishana kwao, kuwa ni alama zenye kuonyesha Upweke wetu na Uwezo wetu. Tukauondoa mwangaza kwenye usiku, na kisionekane kitu. Na alama yake ni giza liso kuwa na jua. Hiyo ni ishara kubwa. Na mchana tukaufanya wa kuangaza. Hapo laonekana jua, ile ishara kuu, ili mpate kwenda mtakako wakati huo katika kutafuta maisha yenu. Na katika kuja usiku na mchana mpate kujua idadi ya miaka na hisabu za miezi na siku. Na Sisi tumekubainishieni kila kitu kwa uwazi kwa sababu ya maslaha yenu, ili isimame hoja juu yenu baada kutimia neema.