وَكُلَّ إِنسَٰنٍ أَلۡزَمۡنَٰهُ طَٰٓئِرَهُۥ فِي عُنُقِهِۦۖ وَنُخۡرِجُ لَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ كِتَٰبٗا يَلۡقَىٰهُ مَنشُورًا ١٣
Wakulla insānin alzamnāhu tā'irahū fī 'unuqihī wanukhriju lahū yawmal-qiyāmati kitāban yalqāhu manshūrā
Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa. 13
Maelezo ya chini
13 Na kila mtu tumemfungamanisha na a'mali yake, vitendo vyake, kama koja lilioko shingoni. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu kilicho andikwa vitendo vyake vyote. Atakiona kitabu hicho kiwazi iwe wepesi kwake kukisoma.