وَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلِيّٞ مِّنَ ٱلذُّلِّۖ وَكَبِّرۡهُ تَكۡبِيرَۢا ١١١
Waqulil-hamdu lillāhil-ladhī lam yattakhidh waladan walam yakul lahū sharīkun fil-mulki walam yakul lahū waliyyum minadh-dhulli wakabbirhu takbīrā
Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa. 111
Maelezo ya chini
111 Nasema Alhamdulillah, Himdi zote, yaani sifa na shukrani, ni za Mwenyezi Mungu ambaye hakuzaa mwana, kwani hamhitajii; wala hana mshirika katika ufalme, kwani Yeye peke yake ndiye aliye uanzisha; wala hana msaidizi wa kumtia nguvu kwa udhaifu fulani unao mpata. Na mtukuze Mola wako Mlezi kwa utukufu mkubwa ulio laiki naye.