Surat Al-Imran, aya 69

3:69

وَدَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يُضِلُّونَكُمۡ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ ٦٩

Waddat tā'ifatum min ahlil-kitābi law yudillūnakum wamā yudillūna illā anfusahum wamā yash'urūn

Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao penda kukupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao, nao wenyewe hawatambui. 69

Maelezo ya chini

69 Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao tamani kuwapotoa Waumini na kuwafitini waache Dini yao, kwa kuwatilia mikorogo ya kudhoofisha itikadi. Lakini katika kazi yao hii hawatampotoa mtu ila nafsi zao wenyewe kwa kuendelea katika upotovu, ambao utakuja kuwagubika wao wenyewe tu, na wala hawajui kuwa matokeo ya juhudi yao ovu yatawapata wenyewe, wala hayatawadhuru Waumini.