Surat Al-Imran, aya 68

3:68

إِنَّ أَوۡلَى ٱلنَّاسِ بِإِبۡرَٰهِيمَ لَلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ وَهَٰذَا ٱلنَّبِيُّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۗ وَٱللَّهُ وَلِيُّ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٦٨

Inna awlan-nāsi bi ibrāhīma lalladhīnat-taba'ūhu wahādhan-nabiyyu walladhīna āmanū wallāhu waliyyul-mu'minīn

Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini. 68

Maelezo ya chini

68 Hakika wenye haki kabisa kunasibiana na Ibrahim na Dini yake ni wale walio mwitikia wito wake na wakaongoka kufuata uwongofu wake katika zama zake, na vile vile Muhammad s.a.w. na walioamini pamoja naye. Kwani hao ni watu wa Tawhidi safi ya kweli, kumwamini Mwenyezi Mungu mmoja bila ya walakini. Hiyo ndiyo Dini ya Ibrahim. Mwenyezi Mungu anawapenda Waumini, na Yeye atawanusuru, kwani wao ni vipenzi vyake, na atawalipa kwa mema na ziada.