فَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَأُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ ٥٦
Fa ammal-ladhīna kafarū fa u'addhibuhum 'adhāban shadīdan fid-dunyā wal-ākhirati wamā lahum min nāsirīn
Ama wale walio kufuru, nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Akhera, wala hawatapata wa kuwanusuru. 56
Maelezo ya chini
56 Ama wale wanao kataa kwa ukafiri nitawaonjesha adhabu ya hizaya na mateso kwa kuwasalitisha mataifa mengine juu yao katika dunia, na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi na ina hizaya zaidi. Na wala hawana wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.