Surat Al-Imran, aya 55

3:55

إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَىٰٓ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَجَاعِلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوكَ فَوۡقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ فِيمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ ٥٥

Idh qālallāhu yā'īsā innī mutawaffīka warāfi'uka ilayya wamutahhiruka minal-ladhīna kafarū wajā'ilul-ladhīnat-taba'ūka fawqal-ladhīna kafarū ilā yawmil-qiyāmati thumma ilayya marji'ukum fa ahkumu baynakum fīmā kuntum fīhi takhtalifūn

Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana. 55

Maelezo ya chini

55 Taja ewe Nabii, pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa Mimi nitakutimizia ajali yako,(yaani nitakufisha kifo cha kawaida kama alivyo sema Ibn Abbas r.a. Taz. Ibn Kathir) wala sitamwezesha mtu yeyote kukuuwa. Nami nitakunyanyua pahala pa utukufu wangu, na nitakuepusha na maadui wako wanao kusudia kukuuwa, na nitawafanya wanao kufuata wasio kengeuka na dini yako, wawe na nguvu na utawala juu ya wale wasio fuata uwongofu wako, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu ni Akhera. Hapo nitawahukumu katika hayo mlio kuwa mkizozana kwayo katika mambo ya dini.