Surat Al-Imran, aya 51

3:51

إِنَّ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ هَٰذَا صِرَٰطٞ مُّسۡتَقِيمٞ ٥١

Innallāha rabbī warabbukum fa'budūhu hādhā sirātum mustaqīm

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabudni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. 51

Maelezo ya chini

51 Kwani hakika Mwenyezi Mungu ametumiminia mimi na nyinyi kila namna ya wema, amenilea mimi na nyinyi, ni Mola Mlezi wenu na wangu mimi. Basi muabuduni Yeye tu. Na hii ndio njia isiyo kwenda ovyo.