۞ فَلَمَّآ أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنۡهُمُ ٱلۡكُفۡرَ قَالَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَٱشۡهَدۡ بِأَنَّا مُسۡلِمُونَ ٥٢
Falammā ahassa 'īsā minhumul-kufra qāla man ansārī ilallāhi qālal-hawāriyyūna nahnu ansārullāhi āmannā billāhi washhad bi annā muslimūn
Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. 52
Maelezo ya chini
52 Basi alipo kuja Isa a.s. akawaita watu wake wafuate Njia Iliyo Nyooka, wengi wao walikataa. Alipo yajua hayo aliwaelekea na kuwaambia: Ni nani atakaye nisaidia katika kazi hii niifanyayo ya kuitia kwenye Haki? Wakamjibu baadhi ya Waumini wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na yeye: Sisi tunakuunga mkono, na tutakusaidia, kwa sababu wewe ni Mwitaji, unaita watu wende kwa Mwenyezi Mungu. Na shuhudia kuwa sisi tumemsafia Mwenyezi Mungu na ni wenye kufuata amri zake.