مِن قَبۡلُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ ٱلۡفُرۡقَانَۗ إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ ٤
Min qablu hudal lin-nāsi wa anzalal-furqāna innal-ladhīna kafarū bi'āyātillāhi lahum 'adhābun shadīdun wallāhu 'azīzun dhuntiqām
Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa. 4
Maelezo ya chini
4 Ameziteremsha hizo kabla ya Qur'ani ili kuwaongoa watu. Walipo kengeuka akaiteremsha Qur'ani ipambanue baina ya Haki na baat'ili, baina ya kweli na uwongo, baina ya uwongofu na upotovu. Basi hii Qur'ani ni Kitabu cha kweli, chenye kudumu milele. Na kila mwenye kuacha aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu na akazikanya Aya zake, Ishara zake, atapata adhabu iliyo kali. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza, hashindwi na kitu, na Mwenye kuwalipa wanao stahiki kulipwa.