إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَخۡفَىٰ عَلَيۡهِ شَيۡءٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ ٥
Innallāha lā yakhfā 'alayhi shay'un fil-ardi walā fis-samā'
Hakika Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, duniani wala mbinguni. 5
Maelezo ya chini
5 Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Kwa hivyo hapana kinacho fichika kwake katika Ardhi na hata katika Mbingu, kikiwa kidogo au kikubwa, kinacho onekana na kisicho onekana.