ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُ ٢
Allāhu lā ilāha illā huwal-hayyul-qayyūm
Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele. 2
Maelezo ya chini
2 Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na kila kiliomo ulimwenguni kinashuhudia hayo kwa namna ya kilivyo umbika na kushikamana, katika umbo na kazi, na viumbe vyenginevyo. Na Yeye Mwenyezi Mungu ni Yuhai, hafi. Ni Mwenye kusimamia na kuendesha mambo yote ya ulimwengu. Yeye ndiye Mwenye kuyadabiri (kuyaendesha) na kuyasarifu.