Surat Al-Imran, aya 178

3:178

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ خَيۡرٞ لِّأَنفُسِهِمۡۚ إِنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِثۡمٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ ١٧٨

Walā yahsabannal-ladhīna kafarū annamā numlī lahum khayrul li anfusihim innamā numlī lahum liyazdādū ithman walahum 'adhābum muhīn

Wala wasidhani wale wanao kufuru kwamba huu muhula tunao wapa ni kheri yao. Hakika tunawapa muhula wazidi madhambi. Na yao wao ni adhabu ya kuwadhalilisha. 178

Maelezo ya chini

178 Wasidhani hao makafiri kuwa vile kuwapururia tunapo wakunjulia umri wao, na tukawapa njia za starehe katika maisha yao ya duniani, kuwa ndio kheri yao. Kwani kuwaongezea umri na kuwakunjulia riziki huwapelekea kudumu na kuchuma madhambi na kuzidi kustahiki adhabu ya kuwafedhehesha aliyo waandalia Mwenyezi Mungu.