وَلَا يَحۡزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡكُفۡرِۚ إِنَّهُمۡ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۚ يُرِيدُ ٱللَّهُ أَلَّا يَجۡعَلَ لَهُمۡ حَظّٗا فِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ ١٧٦
Walā yahzunkal-ladhīna yusāri'ūna fil-kufri innahum lan yadurrullāha shay'an yurīdullāhu allā yaj'ala lahum hazzan fil-ākhirati walahum 'adhābun 'azīm
Wala wasikuhuzunishe wale wanao kimbilia ukafirini. Hakika hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee sehemu yoyote katika Akhera, na yao wao adhabu kubwa. 176
Maelezo ya chini
176 Ewe Nabii! Usihuzunike ukiwaona wale ambao wanazidi ukafiri, na wanawania kuzidisha maovu. Hao hawamletei Mwenyezi Mungu madhara yoyote, kwani Yeye ni Mwenye nguvu juu ya waja wake. Bali Mwenyezi Mungu anataka wasiwe na sehemu yoyote katika thawabu za Akhera, na juu ya kukosa kwao thawabu hizo njema watapata adhabu kubwa.