Surat Al-Imran, aya 175

3:175

إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ يُخَوِّفُ أَوۡلِيَآءَهُۥ فَلَا تَخَافُوهُمۡ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ١٧٥

Innamā dhālikumush-shaytānu yukhawwifu awliyā'ahū falā takhāfūhum wakhāfūni in kuntum mu'minīn

Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini. 175

Maelezo ya chini

175 Mwenyezi Mungu Aliye takasika anawabainishia Waumini kwamba hao wanao kutieni khofu kuogopa kupambana na maadui zenu si lolote ila ni vibaraka wa Shetani anaye watia khofu wafwasi wake awafanye woga. Na nyinyi si katika hao. Basi msiridhie kutishwa, bali mkhofuni Mwenyezi Mungu peke yake kama nyinyi mna Imani ya kweli, na mnasimamia kutimiza yanayo lazimishwa na Imani hiyo.