يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُواْ ٱلرِّبَوٰٓاْ أَضۡعَٰفٗا مُّضَٰعَفَةٗۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ١٣٠
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū lā ta'kulur-ribawā ad'āfam mudā'afatan wattaqullāha la'allakum tuflihūn
Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. 130
Maelezo ya chini
130 Enyi mlio amini! Mkikopesha msichukue katika deni ila rasilmali yenu tu. Msifanye kuzidisha juu ya deni faida ya kuzidi mwaka kwa mwaka ikawa kuzidi juu kwa juu. Msiyale mali ya watu kwa upotovu. Hakika nyinyi mtaongokewa na mtafuzu pindi mkiepukana na riba, ikiwa ndogo au kubwa.