Surat Al-Imran, aya 129

3:129

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ١٢٩

Walillāhi mā fis-samāwāti wamā fil-ardi yaghfiru liman yashā'u wayu'addhibu man yashā'u wallāhu ghafūrur rahīm

Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika Mbingu na vilivyomo katika Ardhi. Yeye humsamehe na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye kurehemu. 129

Maelezo ya chini

129 Bila ya shaka vitu vyote vilioko katika Mbingu na katika Ardhi ni vya Mwenyezi Mungu peke yake, kwa kuviumba na kuvimiliki. Na Yeye ndiye Mwenye uwezo juu ya kila kitu, kila kitu kimo mikononi mwake. Yeye humsamehe ampendaye na akamuadhibu amtakaye. Lakini kusamehe kwake ndiko kulio karibu zaidi, na rehema yake ni ya kutarajiwa sana zaidi. Kwani Yeye hakika ni mwingi wa kusamehe na kurehemu.