Surat Al-Imran, aya 120

3:120

إِن تَمۡسَسۡكُمۡ حَسَنَةٞ تَسُؤۡهُمۡ وَإِن تُصِبۡكُمۡ سَيِّئَةٞ يَفۡرَحُواْ بِهَاۖ وَإِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ لَا يَضُرُّكُمۡ كَيۡدُهُمۡ شَيۡـًٔاۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ ١٢٠

In tamsaskum hasanatun tasu'hum wa in tusibkum sayyi'atun yafrahū bihā wa in tasbirū watattaqū lā yadurrukum kayduhum shay'an innallāha bimā ya'malūna muhīt

Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo. 120

Maelezo ya chini

120 Nyinyi mkipata neema, kama vile kushinda vitani na ngawira, wao husikitika. Mkipata msiba kama ukame na kushindwa, wao hufurahia msiba wenu. Lakini nyinyi mkisubiri juu ya maudhi yao, na mkajizuilia na kule kuwafanya urafiki mliko katazwa, basi maudhi yao na uadui wao hautakudhuruni kitu. Kwani Yeye Aliye tukuka anavijua vyema vitimbi wanavyo vifanya, wala Yeye hashindwi kukulindeni nao.