وَإِذۡ غَدَوۡتَ مِنۡ أَهۡلِكَ تُبَوِّئُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مَقَٰعِدَ لِلۡقِتَالِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ١٢١
Wa idh ghadawta min ahlika tubawwi'ul-mu'minīna maqā'ida lil-qitāli wallāhu samī'un 'alīm
Na pale ulipo toka asubuhi, ukaacha ahali zako uwapange Waumini kwenye vituo kwa ajili ya vita - na Mwenyezi Mungu anasikia na anajua. 121
Maelezo ya chini
121 Na hebu taja Ewe Nabii! Pale ulipo toka asubuhi mapema ukaacha ahali zako, watu wako wa nyumbani, ukenda mpaka Uhud kwa makusudi ya kuwaweka Waumini katika makao yao kwa ajili ya vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia kauli zenu, ni Mwenye kuzijua niya zenu.