Surat Al-Imran, aya 119

3:119

هَٰٓأَنتُمۡ أُوْلَآءِ تُحِبُّونَهُمۡ وَلَا يُحِبُّونَكُمۡ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ كُلِّهِۦ وَإِذَا لَقُوكُمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَوۡاْ عَضُّواْ عَلَيۡكُمُ ٱلۡأَنَامِلَ مِنَ ٱلۡغَيۡظِۚ قُلۡ مُوتُواْ بِغَيۡظِكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ١١٩

Hā'antum ulā'i tuhibbūnahum walā yuhibbūnakum watu'minūna bil-kitābi kullihī wa idhā laqūkum qālū āmannā wa idhā khalaw 'addū 'alaykumul-anāmila minal-ghayzi qul mūtū bighayzikum innallāha 'alīmu bidhātis-sudūr

Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapo kutana nanyi husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao wanakuumieni vidole kwa chuki. Sema: Kufeni kwa chuki yenu! Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo vifuani. 119

Maelezo ya chini

119 Enyi nyinyi Waumini! Mnawapenda hawa makafiri na wanaafiki kwa ajili ya ujamaa, au urafiki au mapenzi tu. Na wao, lakini, hawakupendeni kwa sababu ya kuing'ang'anilia dini yao. Na nyinyi mnaamini Vitabu vyote vilivyo teremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wanapo kutana nanyi hujitia imani ili kukudanganyeni. Na wakisha kuacheni huziuma ncha za vidole vyao kwa chuki na kukasirika. Ewe Nabii! Waambie: Endeleeni na hiyo chuki yenu mpaka mfe! Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyajua yanayo fichikana vifuani, na atakulipeni kwavyo.