Surat Al-Imran, aya 106

3:106

يَوۡمَ تَبۡيَضُّ وُجُوهٞ وَتَسۡوَدُّ وُجُوهٞۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسۡوَدَّتۡ وُجُوهُهُمۡ أَكَفَرۡتُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ ١٠٦

Yawma tabyaddu wujūhun wataswaddu wujūhun fa ammal-ladhīnaswaddat wujūhuhum akafartum ba'da īmānikum fadhūqul-'adhāba bimā kuntum takfurūn

Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika (kuwa nyeusi). Ama hao ambao nyuso zao zitasawijika wataambiwa: Je! Mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mnakufuru. 106

Maelezo ya chini

106 Adhabu kuu hiyo itakuwa Siku zitapo nawiri nyuso za Waumini kwa furaha, na kusawijika kwa masikitiko na huzuni nyuso za makafiri. Wataambiwa kwa kuwatahayarisha: Je, mmekufuru baada ya kuwa mlikulia juu ya Imani na ut'iifu wa haki, na mkaletewa hoja zilizo wazi? Basi onjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri wenu!