وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱبۡيَضَّتۡ وُجُوهُهُمۡ فَفِي رَحۡمَةِ ٱللَّهِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ١٠٧
Wa ammal-ladhīnabyaddat wujūhuhum fafī rahmatillāhi hum fīhā khālidūn
Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu. 107
Maelezo ya chini
107 Ama wale nyuso zao zimekuwa nyeupe, yaani zimenawiri, kwa kufurahi, hao watakuwa katika Pepo ambayo Mwenyezi Mungu amewapa kwa rehema yake, wadumu humo milele.