يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِۦ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسۡلِمُونَ ١٠٢
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanut-taqullāha haqqa tuqātihī walā tamūtunna illā wa antum muslimūn
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu. 102
Maelezo ya chini
102 Hakika mlango wa shari uwazi ikiwa hamumchi Mwenyezi Mungu. Basi enyi mlio amini! Mkhofuni Mwenyezi Mungu kwa khofu inayopasa, kwa kutenda anayo amrisha, na kuyaepuka anayo yakataza. Na dumuni juu ya Uislamu mpaka mtakapo kutana na Mwenyezi Mungu.