وَكَيۡفَ تَكۡفُرُونَ وَأَنتُمۡ تُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ وَفِيكُمۡ رَسُولُهُۥۗ وَمَن يَعۡتَصِم بِٱللَّهِ فَقَدۡ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ ١٠١
Wakayfa takfurūna wa antum tutlā 'alaykum āyātullāhi wafīkum rasūluhū waman ya'tasim billāhi faqad hudiya ilā sirātim mustaqīm
Na vipi mkufuru hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu na Mtume yuko kati yenu? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu basi huyo ameongozwa kwenye Njia Iliyo Nyooka. 101
Maelezo ya chini
101 Hebu izingitieni hali yenu ya ajabu, kuwa mnapotoka na mnakufuru baada ya Imani, na hali mnasomewa Qur'ani, na Mtume mnaye, anakubainishieni na anakukingeni na upotovu katika Dini yenu. Na mwenye kumkimbilia Mola wake Mlezi, na akashikamana na Dini yake, basi huyo amefanya vyema. Mola wake Mlezi amemwongoa kwenye Njia ya kufuzu na kufaulu.