Surat Al-Hijr, aya 82

15:82

وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ ٨٢

Wakānū yanhitūna minal-jibāli buyūtan āminīn

Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani. 82

Maelezo ya chini

82 Nao walikuwa watu wenye nguvu na wajenzi. Walikuwa wakijenga majumba yao katika milima na wakiichonga hiyo hiyo milima. Na wao walikuwa wakijiamini kuwa wametua na nafsi zao na mali yao.