Surat Al-Hijr, aya 16

15:16

وَلَقَدۡ جَعَلۡنَا فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَزَيَّنَّٰهَا لِلنَّٰظِرِينَ ١٦

Walaqad ja'alnā fis-samā'i burūjan wazayyannāhā lin-nāzirīn

Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia. 16

Maelezo ya chini

16 Na Sisi tumeweka mbinguni sayari na nyota, kwa makundi yenye hisabu zake na yenye kukhitalifiana umbo lake na sura yake. Na kadhaalika tukazipamba kwa wenye kuziangalia kwa kutuza na kuzingatia, na kuchunguza kwazo dalili za uwezo wa Muumbaji wao.