مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ كَيۡ لَا يَكُونَ دُولَةَۢ بَيۡنَ ٱلۡأَغۡنِيَآءِ مِنكُمۡۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمۡ عَنۡهُ فَٱنتَهُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ٧
Mmā afā'allāhu 'alā rasūlihī min ahlil-qurā falillāhi walir-rasūli walidhil-qurbā wal-yatāmā wal-masākīni wabnis-sabīli kay lā yakūna dūlata baynal-aghniyā'i minkum wamā ātākumur-rasūlu fakhudhūhu wamā nahākum 'anhu fantahū wattaqullāha innallāha shadīdul-'iqāb
Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 7
Maelezo ya chini
7 Alicho rudisha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake katika mali ya watu wa vijiji hivi bila ya kuwatimua farasi au ngamia, vitu hivyo ni vya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri. Haya ni hivyo ili yasiwe mali yakizunguka katika mikono ya matajiri peke yao katika nyinyi. Na anacho kupeni Mtume katika hukumu basi kishikeni, na anacho kukatazeni basi kiwacheni. Na jilindeni na kughadhibika kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.