Surat Al-Furqan, aya 8

25:8

أَوۡ يُلۡقَىٰٓ إِلَيۡهِ كَنزٌ أَوۡ تَكُونُ لَهُۥ جَنَّةٞ يَأۡكُلُ مِنۡهَاۚ وَقَالَ ٱلظَّٰلِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلٗا مَّسۡحُورًا ٨

Aw yulqā ilayhi kanzun aw takūnu lahū jannatun ya'kulu minhā waqālaz-zālimūna in tattabi'ūna illā rajulam mashūrā

Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale katika hiyo? Wakasema madhaalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliye rogwa. 8

Maelezo ya chini

8 Na hebu lau angeli mtaka amtosheleze chakula cha kutosha asihitajie kuzunguka masokoni, akamtupia khazina kutoka mbinguni ya kutumia, au akamjaalia na bustani ya kumlisha matunda yake? Na wakubwa wa makafiri walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri, wenye kuwapotoa watu wasimuamini Muhammad, na wenye kufanya hila za kuwaingiza shaka Waumini, walisema: Nyinyi hamumfuati ila huyu mtu aliye zugwa akili yake, basi anabwabwatika bila ya kuwa na hakika.