Surat Al-Baqarah, aya 49

2:49

وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ ٤٩

Wa idh najjaynākum min āli fir'awna yasūmūnakum sū'al-'adhābi yudhabbihūna abnā'akum wayastahyūna nisā'akum wafī dhālikum balā'um mir rabbikum 'azīm

Na vile tulipo kuokoeni kwa watu wa Firauni walio kupeni adhabu mbaya, wakiwachinja wana wenu wa kiume na wakawawacha hai wanawake; na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkubwa ulio toka kwa Mola wenu Mlezi. 49

Maelezo ya chini

49 Na kumbukeni katika neema zetu juu yenu kuwa tumekuokoeni kutokana na mateso ya Firauni na wasaidizi wake walio kuwa wakikuonjesheni adhabu kali kabisa, kwa kuwa wakiwachinja wana wenu wanaume - kwa khofu kuwa miongoni mwao atatokea wa kupindua utawala wa Firauni - na wakiwabakisha wanawake ili wawafanye wajakazi wao wa kuwatuma. Na katika adhabu hizi na uteketezaji huu wa umma ni majaribio makuu kutokana kwa Mola wenu, na ni mtihani mkuu kwenu.