وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ ٥٠
Wa idh faraqnā bikumul-bahra fa anjaynākum wa aghraqnā āla fir'awna wa antum tanzurūn
Na tulipo ipasua bahari kwa ajili yenu na tukakuokoeni, tukawazamisha watu wa Firauni, na huku mnatazama. 50
Maelezo ya chini
50 Kumbukeni vile vile katika neema alizo kuneemesheni Mwenyezi Mungu pale tulipo kupasulieni bahari - na tukayagawa maji katikati ili mpate kupita - mkaokoka, Firauni na askari wake wasikupateni. Na kwa fadhila yetu mkavuka na tukawapatiliza adui zenu kwa sababu yenu, tukawazamisha mbele ya macho yenu. Nyinyi mkawa mnawaona wanazama, na bahari ikiwafunika baada ya nyinyi kwisha vuka salama.