فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ ٢٤٩
Falammā fasala tālūtu bil-junūdi qāla innallāha mubtalīkum binaharin faman shariba minhu falaysa minnī wamal lam yat'amhu fa innahū minnī illā manightarafa ghurfata biyadihī fasharibū minhu illā qalīlam minhum falammā jāwazahū huwa walladhīna āmanū ma'ahū qālū lā tāqata lanal-yawma bijālūta wajunūdihī qālal-ladhīna yazunnūna annahum mulāqullāhi kam min fi atin qalīlatin ghalabat fi atan kathīrata bi idhnillāhi wallāhu ma'as-sābirīn
Basi Twaluti alipo ondoka na majeshi alisema: Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo si pamoja nami, na asiye kunywa atakuwa pamoja nami: ila atakaye teka kiasi ya kitanga cha mkono wake. Lakini walikunywa humo isipo kuwa wachache tu miongoni mwao. Alipo vuka mto yeye na wale walio amini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri. 249
Maelezo ya chini
249 Taluti alipo toka nao aliwaambia: "Mwenyezi Mungu anakujaribuni kwa mto ambao mtaukuta njiani mwenu. Msinywe katika mto huo ila tama moja tu. Mwenye kunywa zaidi ya hivyo basi hayumo katika jeshi letu, wala jamii yetu. Kwani amekuwa ameacha kumt'ii Mwenyezi Mungu. Wala asinifuate ila yule ambaye hakunywa ila tama moja tu." Hawakuweza kuvumilia jaribio hili, wakanywa maji mengi, ila wachache tu kati yao. Basi akafuatana na hichi kikundi kidogo akavuka nao mto. Walipoona wingi wa maadui wao walisema: "Hatutoweza hii leo kupigana na Jaluti na askari wake kwa wingi wao na uchache wetu." Baadhi yao wenye nyoyo madhbuti kwa kutaraji kwao malipo ya Mwenyezi Mungu watapo kutana naye, walisema: "Msiogope kitu! Mara nyingi wachache wenye kuamini huwashinda wengi walio makafiri. Subirini, kwani ushindi watapata wenye kusubiri."