Surat Al-Baqarah, aya 248

2:248

وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ءَايَةَ مُلۡكِهِۦٓ أَن يَأۡتِيَكُمُ ٱلتَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَبَقِيَّةٞ مِّمَّا تَرَكَ ءَالُ مُوسَىٰ وَءَالُ هَٰرُونَ تَحۡمِلُهُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ٢٤٨

Waqāla lahum nabiyyuhum inna āyata mulkihī an ya'tiyakumut-tābūtu fīhi sakīnatum mir rabbikum wabaqiyyatum mimmā taraka ālu mūsā wa ālu hārūna tahmiluhul-malā'ikatu inna fī dhālika la'āyatal lakum in kuntum mu'minīn

Na Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni kukuleteeni lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza nyoyo zenu, kitokacho kwa Mola wenu Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina Harun, wanalichukua Malaika. Bila shaka katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini. 248

Maelezo ya chini

248 Na Nabii wao aliwaambia: "Hakika dalili ya ukweli wangu kuwa Mwenyezi Mungu amemteua Twaluti awe ni mtawala wenu ni kuwa atakurejesheeni sanduku la Taurati mlio nyang'anywa, linalo bebwa na Malaika. Na ndani yake yamo baadhi ya mabaki ya watu wa Musa na watu wa Harun walio kuja baada yao. Na likiletwa sanduku hilo nyoyo zenu zitatua. Katika hayo hakika pana dalili ambazo zitakupelekeeni kumfuata na kumridhia, ikiwa kama kweli nyinyi mnataka Haki na mnaiamini."