وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَدۡ بَعَثَ لَكُمۡ طَالُوتَ مَلِكٗاۚ قَالُوٓاْ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ عَلَيۡنَا وَنَحۡنُ أَحَقُّ بِٱلۡمُلۡكِ مِنۡهُ وَلَمۡ يُؤۡتَ سَعَةٗ مِّنَ ٱلۡمَالِۚ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰهُ عَلَيۡكُمۡ وَزَادَهُۥ بَسۡطَةٗ فِي ٱلۡعِلۡمِ وَٱلۡجِسۡمِۖ وَٱللَّهُ يُؤۡتِي مُلۡكَهُۥ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ ٢٤٧
Waqāla lahum nabiyyuhum innallāha qad ba'atha lakum tālūta malikan qālū annā yakūnu lahul-mulku 'alaynā wanahnu ahaqqu bil-mulki minhu walam yu'ta sa'atam minal-māli qāla innallāhastafāhu 'alaykum wazādahū bastatan fil-'ilmi wal-jismi wallāhu yu'tī mulkahū man yashā'u wallāhu wāsi'un 'alīm
Na Nabii wao akawaambia: Mwenyezi Mungu amekuteulieni Twaluti (Sauli) kuwa ni mfalme. Wakasema: vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tuna haki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa mali? Akasema: Mwenyezi Mungu amemteua yeye juu yenu na amemzidishia ukunjufu wa ilimu na kiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi. 247
Maelezo ya chini
247 Nabii wao akawaambia: "Hakika Mwenyezi Mungu amekuitikieni, basi amemkhiari Twaluti awe ndiye mtawala wenu." Wakuu wao wakapinga huo uteuzi wa Mwenyezi Mungu, wakisema: "Kwa nini awe yeye ni wa kututawala na hali sisi ni bora kuliko yeye. Yeye si mtu wa ukoo bora wala hana mali." Nabii wao akawarudi kwa kusema: "Mwenyezi Mungu amemkhiari yeye kuwa ni mtawala wenu kwa sababu ana sifa nyingi za uwongozi, kama mazoezi makubwa katika mambo ya vita, na siyasa ya kutawala, pamoja na nguvu za mwili. Na utawala uko katika mkono wa Mwenyezi Mungu humpa amtakaye katika waja wake, wala yeye hatagemei urithi wala mali." Na fadhila za Mwenyezi Mungu na ujuzi wake umeenea. Yeye huchagua lilio na maslaha yenu.