Surat Al-Baqarah, aya 137

2:137

فَإِنۡ ءَامَنُواْ بِمِثۡلِ مَآ ءَامَنتُم بِهِۦ فَقَدِ ٱهۡتَدَواْۖ وَّإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا هُمۡ فِي شِقَاقٖۖ فَسَيَكۡفِيكَهُمُ ٱللَّهُۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ١٣٧

Fa in āmanū bimithli mā āmantum bihī faqadihtadaw wwa in tawallaw fa innamā hum fī shiqāqin fasayakfīkahumullāhu wahuwas-samī'ul-'alīm

Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi. 137

Maelezo ya chini

137 Wao wakiamini imani inayo wafikiana na imani yenu basi kweli wameongoka. Lakini wakikakamia katika inadi yao na kukataa kwao basi hao wamo katika ushindani usio koma, na hawana masikizano nanyi. Mwenyezi Mungu atakutosheni kukulindeni na shari yao, ewe Nabii. Na atakupumzisha na ghasia zao za inadi na upinzani wao. Kwani Yeye ni Mwenye kuyasikia wayasemayo, na Mwenye kuyajua hata yaliomo vifuani mwao.