Surat Al-A'raf, aya 6

7:6

فَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلَّذِينَ أُرۡسِلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ٦

Falanas'alannal-ladhīna ursila ilayhim walanas'alannal-mursalīn

Na kwa yakini tutawauliza wale walio pelekewa Ujumbe, na pia tutawauliza hao Wajumbe. 6

Maelezo ya chini

6 Na Siku ya Kiyama hisabu ya Mwenyezi Mungu itachungua kila kitu kwa uadilifu. Tutawauliza watu tulio watumia Mitume: Je, Ujumbe umewafikilia? Na wamewajibu nini hao Wajumbe tulio watuma? Na tutawauliza Mitume pia: Je, mmefikisha yaliyo teremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi? Na hao kaumu zenu wamekujibuni nini?