Surat Al-A'raf, aya 7

7:7

فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيۡهِم بِعِلۡمٖۖ وَمَا كُنَّا غَآئِبِينَ ٧

Falanaqussanna 'alayhim bi'ilmin wamā kunnā ghā'ibīn

Tena tutawasimulia kwa ilimu; wala Sisi hatukuwa mbali . 7

Maelezo ya chini

7 Na tutawapa wote khabari ya kweli yote yaliyo kuwa kwao, kwa sababu hakika Sisi tumewadhibitia kila kitu chao, kwani Sisi hatukuwa mbali nao, wala hatukuwa hatujui waliyo kuwa wakiyafanya.