فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ ٢٢
Fadallāhumā bighurūrin falammā dhāqash-shajarata badat lahumā saw'ātuhumā watafiqā yakhsifāni 'alayhimā min waraqil-jannati wanādāhumā rabbuhumā alam anhakumā 'an tilkumash-shajarati wa aqul lakumā innash-shaytāna lakumā 'aduwwum mubīn
Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri? 22
Maelezo ya chini
22 Basi akawachochea kwa udanganyifu mpaka wakenda kula ule mti. Walipo uonja tupu zao zikafichuka, wakaingia wanakusanya majani ya miti kujisitiri tupu zao. Mola wao Mlezi akawakaripia, na akawatanabahisha makosa yao kwa kuwambia: Mimi sikukukatazeni mti ule, na nikakwambieni kuwa Shetani ni adui yenu wa dhaahiri, hakutakieni kheri?