وَيَٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٩
Wayā'ādamuskun anta wazawjukal-jannata fakulā min haythu shi'tumā walā taqrabā hādhihish-shajarata fatakūnā minaz-zālimīn
Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu 19
Maelezo ya chini
19 Na ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika makao ya ukarimu wangu, nayo ndiyo hiyo Bustani, mneemeke humo, mkila kila chakula mpendacho, isipo kuwa mti huu. Msiukaribie! Msije mkawa wenye kujidhulumu nafsi zenu kwa adhabu itayo kupateni kwa kuvunja amri.