أَوۡ تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أَشۡرَكَ ءَابَآؤُنَا مِن قَبۡلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةٗ مِّنۢ بَعۡدِهِمۡۖ أَفَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ ١٧٣
Aw taqūlū innamā ashraka ābā'unā min qablu wakunnā dhurriyyatam mim ba'dihim afatuhlikunā bimā fa'alal-mubtilūn
Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walio shirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao. Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyo yafanya wapotovu? 173
Maelezo ya chini
173 Au mtasema: Walishiriki baba zetu kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tumewafuata tu. Basi ewe Mola Mlezi wetu! Unatushika utuhiliki kwa walio yafanya wapotovu miongoni mwa baba zetu, kwa kujenga misingi ya ushirikina tulio endelea nao? Basi hamna hoja.