وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ ١٦٤
Wa idh qālat ummatum minhum lima ta'izūna qawmanillāhu muhlikuhum aw mu'addhibuhum 'adhāban shadīdan qālū ma'dhiratan ilā rabbikum wala'allahum yattaqūn
Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu. 164
Maelezo ya chini
164 Na wakumbushe pia hao Mayahudi pale kikundi cha watu wema katika wenzao walio tangulia, ambao hawakutenda mabaya waliyo yatenda wengineo, walipo waambia wanao wapa mawaidha wale waovu: Kwa sababu gani mnawapa nasaha watu ambao Mwenyezi Mungu atawahiliki, au atawaadhibu adhabu kali Akhera, kwa sababu ya madhambi wanayo yatenda? Wakasema: Tunawapa mawaidha ili tupate udhuru kwa Mola wako Mlezi, tusiwe tumefanya taksiri, na kutaraji huenda wakamchamngu.