Surat Al-Anfal, aya 3

8:3

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ ٣

Alladhīna yuqīmūnas-salawāta wamimmā razaqnāhum yunfiqūn

Hao ambao wanashika Swala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku. 3

Maelezo ya chini

3 Na hao Waumini walio wa kweli katika Imani, wanashika Swala kwa kutimiza nguzo zake, na kukamilisha unyenyekevu na ut'iifu, ili wawe daima katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na wanatoa katika mali aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la, kwa ajili ya Jihadi, na mambo yote ya kheri, na kuwasaidia wanyonge.