Surat Al-Anfal, aya 2

8:2

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ ٢

Innamal-mu'minūnal-ladhīna idhā dhukirallāhu wajilat qulūbuhum wa idhā tuliyat 'alayhim āyātuhū zādathum īmānan wa'alā rabbihim yatawakkalūn

Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 2

Maelezo ya chini

2 Ama hakika Waumini wa haki na kweli daima wanakuwa na khofu na ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu. Akitajwa Allah Subhanahu, Mwenyezi Mungu Aliye takasika, nyoyo zao hufazaika, na zikajaa khofu. Kwa hivyo kila wakisomewa Aya za Qur'ani Imani yao inazidi kuwa imara, na wao huzidi unyenyekevu na ujuzi, na wala hawamtegemei yeyote ila Mwenyezi Mungu aliye waumba, na ndiye anaye walinda na kuwaendeleza.