وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ أَنتُمۡ قَلِيلٞ مُّسۡتَضۡعَفُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ تَخَافُونَ أَن يَتَخَطَّفَكُمُ ٱلنَّاسُ فَـَٔاوَىٰكُمۡ وَأَيَّدَكُم بِنَصۡرِهِۦ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ٢٦
Wadhkurū idh antum qalīlum mustad'afūna fil-ardi takhāfūna an yatakhattafakumun-nāsu fa'āwākum wa ayyadakum binasrihī warazaqakum minat-tayyibāti la'allakum tashkurūn
Na kumbukeni mlipo kuwa wachache, mkionekana wanyonge katika nchi, mnaogopa watu wasikunyakueni, naye akakupeni pahala pazuri pa kukaa, na akakutieni nguvu kwa nusura yake, na akakupeni riziki nzuri ili mpate kushukuru. 26
Maelezo ya chini
26 Na hebu kumbukeni, enyi Waumini, katika hali ya kuwa mna nguvu, pale mlipo kuwa wachache na wanyonge. Maadui walikudhilini kwa unyonge wenu, nanyi mlishikwa na khofu wasije maadui zenu kukunyakueni. Basi tena mkahama kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yenu yakawa Yathrib (Madina). Na mkapata manusura kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na tawfiki yake, na akakuruzukuni ngawira njema kutaraji mtashukuru kwa neema hii, na muendelee katika Njia ya Jihadi kulinyanyua Neno la Haki.