Surat Al-Anfal, aya 25

8:25

وَٱتَّقُواْ فِتۡنَةٗ لَّا تُصِيبَنَّ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمۡ خَآصَّةٗۖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ٢٥

Wattaqū fitnatal lā tusībannal-ladhīna zalamū minkum khāssatan wa'lamū annallāha shadīdul-'iqāb

Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 25

Maelezo ya chini

25 Na jikingeni na Dhambi kubwa ya kufisidi jamii yenu, kama vile kuacha kwenda kwenye Jihadi, na kufarikiana mkagawana mapande mapande, na kama kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu. Kwani Fitna hiyo, Dhambi hiyo, haiwapati wale walio dhulumu peke yao, bali inawapata wote. Na mjue kuwa bila ya shaka kuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali hapa duniani na Akhera pia.