Surat Al-Anfal, aya 20

8:20

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَأَنتُمۡ تَسۡمَعُونَ ٢٠

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū atī'ullāha warasūlahū walā tawallaw 'anhu wa antum tasma'ūn

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe naye, nanyi mnasikia. 20

Maelezo ya chini

20 Enyi mlio isadiki Haki, na mkaifuata! Hakika mmejua ushindi umepatikana kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kumt'ii Mtume wake. Basi endeleeni kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume. Wala msiupuuze wito wa Mtume anao itia Haki, nanyi mnamsikia na mnafahamu ayasemayo.