Surat Al-Anbiya, aya 26

21:26

وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۚ بَلۡ عِبَادٞ مُّكۡرَمُونَ ٢٦

Waqālut-takhadhar-rahmānu waladan subhānahū bal 'ibādum mukramūn

Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, ana mwana! Subhanahu, Ametakasika na hayo! Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa. 26

Maelezo ya chini

26 Na baadhi ya makafiri wa Kiarabu walisema: Arrahman, Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, ana mwana, kwa yale madai yao kuwa Malaika ni binti za Mwenyezi Mungu. Ametakasika na kuwa na mwana! Kwani hao Malaika ni waja wake walio tukuzwa tu kwa kuwakaribisha, na kwa wanavyo muabudu Yeye.