Surat Al-An'am, aya 68

6:68

وَإِذَا رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ يَخُوضُونَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَلَا تَقۡعُدۡ بَعۡدَ ٱلذِّكۡرَىٰ مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ ٦٨

Wa idhā ra'aytal-ladhīna yakhūdūna fī āyātinā fa a'rid 'anhum hattā yakhūdū fī hadīthin ghayrihī wa immā yunsiyannakash-shaytānu falā taq'ud ba'dadh-dhikrā ma'al-qawmiz-zālimīn

Na unapo waona wanao ziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shet'ani akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu. 68

Maelezo ya chini

68 Na ukihudhuria katika baraza za makafiri, ukawakuta wanazikosoa Aya za Qur'ani, au wanazifanyia maskhara, basi wewe waepuke mpaka watapo ingia katika mazungumzo mengine. Na ukisahau na ukakaa nao wakati wa mazungumzo yao hayo mapotovu, kisha ukaikumbuka amri ya Mwenyezi Mungu ya kujitenga nao, basi usikae tena na watu madhaalimu baada ya kukumbuka.